FANYENI KAZI KWA WELEDI NA UADILIFU......

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa akifungua Mkutano Mkuu wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodomma leo. Picha zote na Othman Michuzi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodomma leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodomma leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania, Zuhura Maganga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodomma leo.


Na Janeth Raphael - Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza Makatibu mahsusi kwa ubunifu mwingi walionao katika kazi zao.

Rais Samia ameyasema hayo leo june 2022 katika Mkutano mkuu wa tisa wa kitaaluma wa makatibu mahsusi Tanzania uliofanyika Dodoma.

Rais amesema TAPSEA imekuwa, idadi imeongezeka sana "Taasisi imeongezeka sana hasa makatibu wanaume na makatibu mahsusi kutoka Zanzibar idadi ilikuwa chini tulipokutana kwenye mkutano mwaka 2017 hongereni sana" - Rais Samia.

RAIS amesema serikali inatambua majukumu ya Makatibu mahsusi ni muhimu mno na huwa anajiuliza wasingekuwepo wao wangekuwa wanafanyaje kazi zao

"Fanyeni kazi kwa weledi na uadilifu unapokosa haya mawili unakuwa tu mpiga chapa jiheshimu na heshimu kazi yako na sehemu zenu za kazi, fanyeni kazi kwa wakati na zaidi mtunze Siri zaw mabosi wenu na sehemu zenu za kazi kwa ujumla" Amesema Rais Samia.

Aidha Rais Samia amewataka mabosi kutenga bajeti za kuwaendeleza kimasomo, semina, mikutano na mafunzo mbalimbali kwa makatibu mahsusi asiwepo wa kuachwa nyuma.

"Naagiza chuo cha uhazili Cha Tabora kiwe maalumu kwa uzalishaji wa makatibu mahsusi watakaohudumia ofisi za Serikali." Rais Samia.

Hata hivyo Rais amemtaka mwenyekiti wa chama cha watunza kumbukumbu na makatibu mahsusi wawe makini na kazi zao Kwa kuwa nyaraka sa Serikali zinakutwa mitandaoni, Siri zinaanikwa waziwazi wawe makini na jambo hilo Kwa kuwa usalama wa Serikali upo mikononi mwao na hawatokubali kusalitiwa.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala bora, Mhe Jenista Mhagama amemshukuru Rais kwa kutekeleza ahadi yake aliyoahidi mwaka jana akiwa Bungeni kwenye hotuba yake aliyosema ataboresha maslahi ya watumishi wa umma.

Kwa upande mwingine Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe Innocent Bashunguwa Amesema kuna baadhi ya waajiri wasiotenda haki kwa makatibu mahsusi hivyo amewaelekeza wakurugenzi wote nchini kwenye Wizara, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa kuwa ole wao kwa yeyote atakayewazuia makatibu mahsusi kushifiki kwenye fursa zinazowahusu Kama vile mafunzo na semina.

Wakati huo huo naye mwenyekiti wa Chama cha Makatibu mahsusi Tanzanania (TAPSEA) Zuhura Maganga amesema lengo na madhumuni ya umoja huo ni kuwaweka pamoja na kukuza taaluma zao Kwani umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments