Kabaka ametoa rai hiyo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho, ambapo amesema wanapaswa kuwa wamoja na kuepuka makundi.
"Niwatake muwe na umoja na kusiwe na makundi, wanawake tukigawanyika tukiwa na makundi, nchi nzima itakuwa na makundi, chama kitakuwa na makundi, na jeshi lenye makundi haliwezi kushinda," amesema.
Mwenyekiti huyo pia amekagua na kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya Katibu wa UWT Mkia wa Kilimanjaro na wilaya ya Moshi Mjini, ambapo ameahidi kuchangia Sh4 milioni, katika katika ujenzi wa nyumba hizo ambazo zitagharimu Sh150 milioni hadi kukamilika.
Katibu wa chama cha mapinduzi Mkoa wa kilimanjaro, Jonathan Mabihya amesema chama kitahakikisha kinadhibiti na kuchukua hatua kwa wapanga safu wote katika kipindi hiki cha uchaguzi ndani ya chama.
"Hatutasita kuchukua hatua kwa wale wote wanaopanga safu na wale wote wanaokiuka taratibu za uchaguzi wa chama na jumuiya zetu," amesema mabihya.
0 Comments