KAMPENI YA SMAUJATA KUWAFIKIA WANANCHI 400,000 MKOA WA SINGIDA NDANI YA MIEZI MINNE


Kaimu Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Singida, Emanuel Digha, akiinadi kampeni mpya ya kupinga ukatili wa kijinsia inayoitwa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) kwa Wananchi na Viongozi wa Kata ya Mandewa katika mkutano wa hadhara wa kujadili maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya cha kata hiyo.


Viongozi wa kampeni ya SMAUJATA wakiwa kwenye mkutano huo.


Viongozi wa SMAUJATA wakiwavika nembo ya kupinga ukatili ya kijinsia Diwani wa Kata hiyo, Baraka Hamisi na Kaimu Afisa Mtendaji Kata ya Mandewa, Mwanahali Said katika mkutano huo.

Diwani wa Kata ya Mandewa, Baraka Hamisi, akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mandewa katika mkutano wa kujadili maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha kata hiyo.


Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Anwar Milulu, akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mandewa katika mkutano wa kujadili maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha kata hiyo.


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mandewa, Yusuph Kijanga akizungumza kwenye mkutano huo wa Wananchi wa kata hiyo kujadili maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya..

Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Singida, Tumaini Sabbi akizungumza kwenye mkutano huo.
Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Mandewa, Mwanahali Said akiongoza mkutano huo.

Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa Kata ya Mandewa, Mohamed Muna (Maarufu Muna Dalali) akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.


Mkutano ukiendelea.

Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Mandewa, Mwanahali Said akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Mandewa, Baraka Hamisi wakati wa mkutano huo. 

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mandewa, Yusuph Kijanga (aliyeshika maiki nyuma kushoto) akiwatambulisha viongozi wa CCM wa kata hiyo.

KAMPENI ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Singida imedhamilia kuwafikiwa  wananchi 400,000 ili kuwapa elimu ya namna kupinga na kuufuta kabisa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia unaoikumba jamii hapa nchini.

Kaimu Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Singida, Emanuel Digha, akizungumza katika mkutano wa wananchi wa kata ya Mandewa uliofanyika mtaa wa Mwaja, Manispaa ya Singida alisema watu hao watafikiwa katika kipindi cha ndani ya miezi mitatu hadi minne ijayo.

Alisema mbinu zinazotumika katika kutoa elimu ni kuhudhuria mikutano ya hadhara, kutembelea shule, kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamiii na kwamba wananchi wanapaswa kuunga mkono kampeni hii ili kukomesha vitendo vya ukatili.

Digha alisema vitendo vya ukatili vingi vinatokana na uelewa mdogo wa jamii ambapo baadhi wamekuwa wakidanganywa na waganga wa kienyeji kwamba wakifanya jambo fulani la ukatili pengine watapata utajiri kitu ambacho ni imani potofu.

Alisema ili kuhakikisha elimu ya kupinga ukatili inawafikia kwa uharaka jamii, SMAUJATA Mkoa wa Singida  ipo mbioni kupata viongozi kuanzia ngazi za mitaa, vitongoji na vijiji ambao watakuwa na jukumu la kuwaelimisha wananchi kuachana na vitendo vya ukatili.

" Nawaasa wananchi vitendo vya ukatili sio vizuri maana sisi tumepewa maisha bure na Mungu kwa hiyo tuache ukatili ili kila mtu aishi na kufanya kazi zake kwa uhuru," alisema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoani hapa, Ambwene Kajula, alisema kampeni hiyo imekuja wakati mwafaka kwani makundi mengi yanakumbana  na ukatili lakini yanaogopa kutoa taarifa ikiwemo kundi la watoto na wazee ambao mara nyingine
hukatiliwa kutokana na imani potofu kama kuhisiwa na vitendo vya ushirikina.

"Nawasihi hata wanaume ambao hupigwa na wake zao lakini wamekuwa hawasemi, hivyo basi kupitia kampeni hii tukishirikiana kutoa taarifa itakuwa msaada mkubwa sana," alisema.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida, Vicent Mafuru alisema kuwa  wao kama wanaharakati wataufikia mkoa wa Singida kuanzia ngazi ya halmshauri, kata,vitongoji hadi vijiji na mitaa ili kutoa elimu na misaada mbalimbali ya namna ya kukabiliana ukatili wa kijinsi ili kulifanya taifa la Tanzania kuwa endelevu katika nyanja zote za kijamiii na kiuchumi.

Mafuru alisema jamiii mkoani hapa inatakiwa kutoa taarifa zinazohusu ukatili dhidi yao hasa wakati  huu wa utekelezaji wa kampeni ya kupinga ukatilii.

“Wanajamiii wanatakiwa kutoa taarifa za matendo maovu yanayoendelea katika nyumba zao,  shuleni na maeneo yote ambayo watu wanakumbana na kaadhia ya unyanyasaji na ukatili kwa kupiga namba 116 na atapata msaada, ” alisema Mafuru.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments