KATIBU ITIKADI NA UENEZI CCM AWATOLEA UVIVU WAPANGA SAFU CCM, ATOA NENO KWA WANACHAMA

 Katibu  wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amewataka wanachama wa Chama hicho kuacha tabia ya kupanga safu za uongozi na kwamba hali hiyo haijengi bali inabomoa.


Shaka ametoa kuali hiyo leo Juni 4,2022 baada ya kushiriki ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Mdimba wilayani Tandahimba mkoani Mtwara ambapo akiwa hapo amewaambia Wanachama wa Chama hicho kuwa Wilaya hiyo inaongoza kwa kupanga safu kwenye uchaguzi unaendelea ndani ya CCM.

"Tuko kwenye uchaguzi wa ndani ya Chama, hapa Tandahimba hamzungumzwi vizuri ,mnapanga safu mno, safu za viongozi zinapangwa, madiwani, wabunge na viongozi wengine acheni kupanga safu ,waachieni wanachama wafanye maamuzi nani wanamtaka,nani hawamtaki.Kila Mwanachama wa Chama hiki ana haki ya kuchaguliwa na kuchagua .Wapeni fursa watimize demokrasia ndani ya Chama chao.

"Dhana ya kuwapangia watu kwa kuangalia mbele tunakokwenda hamjengi Chama,mnakibomoa , niwaombe sana ndugu zangu msikubali kupangwa kwa mafungu ,eti huyu chukua nafasi fulani,chukua nafasibfulani uje unisaidie ,nani anauhakika na kesho? Kuna mtu anauhakika na kesho?

"Tujenge Chama, tusibomoe chama kila mwanachama asizuie wala asitokee kiongozi yoyote kuzuia fomu ya kuwapa wanachama kuomba fomu ya kuomba uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi , huu ni mwaka wa uchgauzi na tunapanga safu ya kusaidia 2024,2025.

"Kupanga safu ndani ya Chama hiki ni kukwamisha harakati za CCM kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi mwaka 2024/2025, na wanaopanga safu hatutawavumilia ,iwe kiongozi wa ngazi yoyote hatutamvumilia atuvurugie Chama na sisi tunaangalia macho,

"Hapa Wilaya ya Tandahimba mmetajwa kwenye jambo hilo kuna upangaji wa safu, hatukubali uwapange wenzio kama nyanya, wee kaa hapa ,wee kaa hapa,hiyo biashara haiko kwenye Chama hiki, kila mmoja anahaki inayoendama na wajibu na kila wajibu unaendana na haki.Timizeni wajibu wenu wa Kikatiba ,timizeni haki zenu ya kikatiba,"amesema Shaka.

Ameongeza ukiwa mwanachama nenda kagombee nafasi yoyote unayotaka huku akifafanua kwamba Uchaguzi ndani ya Chama upo kwenye ngazi ya Kata hivyo anayeweza akagombee, anayeweza kugombea Wilaya akagombee na anayeweza kugombea ngazi ya Mkoa aende kugombea.

"Kama unaweza taifani nenda kagombee ,Chama pamoja na Jumuiya zake hakuna mwenye hatimiliki ndani ya Chama Cha Mapinduzi.Wala hakuna mtu aliyeachiwa urithi na baba yake kwamba wewe tunakuachia urithi. Ndani ya Chama hiki wote mnahaki sawa,niwaombe sana hasa akina mama jitokezeni kuomba nafasi ndani ya Chama cha Mapinduzi.

"Niwaombe sana hasa vijana jitokezeni kwa wingi kuomba nafasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi.Lakini na wazee na ninyi msiwe nyuma kuomba nafasi ndani ya Chama pamoja na Jumuiya iya zake, mchango wenu ni mkubwa ndani ya Chama hiki , Mchango wenu mnahitajika ili tusukume mbele gurudumu la maendeleo,"amesema.

Ameongeza kuwa wao ndio wenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama hiki,hivyo wachague viongozi bora na sio bora viongozi wakuja kukikwamisha Chama huko tunakokwenda.Tunataka viongozi ambao watakuwa na uthubutu ,tunataka viongozi ambao watakuwa na uchungu na wananchi ambao wanawachagua ili kuja kusimamia maslahi ya Chama Cha Mapinduzi."

Katika hatua nyingine Shaka ametumia nafasi hiyo kuzungumzia ujenzi wa Ofisi ambapo ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya Ofisi hiyo. Nimefurahi sana kuja kuweka jiwe la msingi katika Ofisi hii ya Kata na nimeambiwa mzee Kinana ambaye ni Makamu Mwenyekiti wetu alipita hapa, sasa mimi nataka niwahakikishie mzee aliweka ahadi ya kupaua, hiyo ahadi tutaiteikeleza.
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments