KATIBU MKUU CCM AKEMEA TABIA KUWAPANGIA WATUMISHI WAPYA KWA UPENDELEO

 Chama Cha Mapinduzi(CCM) kupitia Katibu Mkuu wake Daniel Chongolo kimekemea tabia ya baadhi ya watendaji wa Serikalib kuwapangia watumishi wapya vituo vya kazi kwa upendeleo.


Akizungumza leo Juni 3, 2022 baada ya kupokea taarifa ya upungufu wa watumishi wa afya na Elimu katika baadhi ya vituo vya afya na Shule wilayani Busega Chongolo ametumia nafasi hiyo kueleza ni vema tabia ya kupeleka watumishi wapya kwenye vituo vya kazi kwa upendeleo ikaachwa na kila mtu anawajibu wa kufanya kazi popote.

Amesema kwamba wananchi katika mahali walipo wanahitaji kuhudumiwa.”Acheni urasimu wapelekeni watumishi wapya kwenye vituo vya kazi vyenye uhitaji acheni kuwarundika Sehemu moja" amesisitiza Chongolo.

Chongolo yupo Wilayani Busega mkoani Simiyu katika muendelezo wa ziara ya kikazi inayolenga kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akizungumza leo Juni 3, 2022 baada ya kupokea taarifa ya upungufu wa watumishi wa afya na Elimu katika baadhi ya vituo vya afya na Shule wilayani Busega

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Wafuasi na Wanachama wa CCM wakati wa mapokezi Kiwilaya kata ya Mkula jimbo la Busega, wilaya ya Busega akitokea Bariadi mkoani Simiyu leo Juni 3, 2022.

Ndugu Chongolo anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Simiyu ambapo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha na kuhimiza uhai wa chama kuanzia ngazi ya mashina.

Chongolo ambaye ameambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ngemela Lubinga atazungumza na wanachama wa Chama hicho pamoja na kukagua miradi ya maendeleo kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya uchgauzi Mkuu mwaka 2020-2025.

Furaha ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo ndani ya jimbo la Busega
Mbunge wa jimbo la Busega Mhe Simon Nyakoro Sirro akieleza mambo mbalimbali ikiwemo changamoto ya upungufu wa Watumishi wa Afya,changamoto ya Kiboko mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisomewa taarifa ya mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Mkula wilayani Busega kutoka kwa Mganga mkuu wa wilaya ya hiyo Dkt.Godfrey Mbagali wakati akiendelea na ziara yake wilayani Busega mkoani Simiyu.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikagua ujenzi wa kituo Cha Afya Cha Mkula wilayani Busega huku akipata maelezo kutoka Kwa Mganga mkuu wa wilaya ya hiyo Dk.Godfrey Mbagali wakati akiendelea na ziara yake wilayani Busega mkoani Simiyu.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiendelelea kukagua toka kukagua kituo cha afya Mkula wilayani Busega.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akitoka kukagua kituo cha afya Mkula wilayani Busega.


Baadhi ya Madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Kabita Mwl. Michael Joseph Halali wakati alipowasili katika shule ya Sekondari ya Kabita katika kata ya Kabita wilayani Busega kujionea ukamilishwaji wa madarasa yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO,ambapo Serikali imetoa Milioni 280 kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments