KERO SUGU ZATATULIWA IKUNGI

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro amemaliza kero muda mrefu ya stendi ya Makiungu kwa kutoa maelekezo ndani ya siku tano ofisi ya mkurugenzi kwa kushirikiana na uongozi wa kata ya mungaa kuifungua stendi hiyo uku marekebisho mengine yakiendelea

Dc Muro ambae amesikiliza na kutatua kero za kata ya mungaa na makiungu amesema kufunguliwa kwa stendi kutasaidia wananchi na wasafirishaji kuwa na eneo huru la kufanyia shughuli zao hatua ambayo pia itaongeza mapato ya halmashauri kutokana na kuwa na udhibiti wa karibu

Dc Muro amesema kwa kuanzia watatumia miundombinu ya vyoo iliyopembeni ambayo itatumiwa pamoja na soko kutokana na kutokuwa na wafanyabiashara wengi uku akiagiza kuwekwa kwa uzio wa mbele wa waya utakaonyesha eneo la magari kuingia na kutokea

Awali Dc Muro alipata nafasi ya kufanya kikao cha ndani na madiwani, watendaji wa kata na vijiji pamoja na halmashauri za vijiji vilivyopo kata ya mungaa na makiungu na kumaliza kwa pamoja changamoto ya bodi ya maji inayohudumia vijiji vitatu katika eneo

Pamoja na mambo mengine Dc Muro amewaelekeza watendaji wa kata na vijiji pamoja na madiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji njia bora ya kuwafuata na kuwahudumia wananchi pamoja na kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo yao
Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi

Post a Comment

0 Comments