Kiongozi wa Mwenge agoma kuzindua miradi tisa Tanga

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2022, Sahili Nyanzabara Geraruma amegoma kuzindua miradi 9 kati ya 82 yenye thamani ya zaidi ya Sh33 bilioni mkoani Tanga kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Juni 6 na Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Kilimanjaro katika kijiji cha Bendera kilichopo katika mpaka wa Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro.

Amesema miongoni mwa miradi ambayo haijazinduliwa ni vyumba vya madarasa, miradi ya maji, ujenzi wa vituo vya afya, mradi wa ujenzi wa kituo cha mafuta pamoja na zahanati.

"Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika katika hatua ya kukabidhi Mwenge huu wa uhuru katika Mkoa wa Kilimanjaro, wakati Mwenge ukiwa mkoani Tanga, ulifanya kazi ya kutembelea, kukagua, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kati ya miradi 82 iliyofanyiwa kazi na Mwenge wa Uhuru haukuridhia kufanya shughuli iliyokusudiwa katika miradi 9," amesema Malima

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments