LAIGWANANI TAUWO: ASANTE MUNGU KWA KUTUPA MSOMERA

 Mkuu wa Kimila wa kabila la Maasai waliokuwa wakiishi katika Hifadhi ya Ngorogoro, Laigwanani Matigoi Tauwo amemshukuru Mungu kwa kumuongoza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuwapatia Makazi Bora katika Kijiji Cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni Tanga.


Akishukuru kwa niaba ya wananchi wenzake wa Ngorogoro ambao wameamua kuhama kwa hiyari yao, Laigwanani Tauwo amesema sasa maisha yao yatakuwa ya amani zaidi na yenye maendeleo kuliko huko nyuma kwa kuwa Serikali imewapatia Nyumba, Ardhi kwa ajili ya Killimo na Ufugaji, pia huduma bora za kijamii kama elimu na afya.

"Namshukuru sana Mungu kwa kutupa Rais Mama Samia, leo sisi tunamiliki nyumba jamani, kweli Mungu mkubwa sana, tunaahidi tutaishi vizuri sana na ndugu zetu wa hapa msomera" amesema Laigwanani Tauwo.

Katika zoezi la kuwapokea wananchi hao walioamua kuhamia Kijiji Cha Msomera ili kupisha shughuli za uhifadhi Ngorongoro, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewakabidhi wananchi hao hati za Ardhi zilizotolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.





 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments