Meya wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani iliyopo Mkoani Mtwara Shadida Ndile amewataka Madiwani pamoja na viongozi wa Halmashauri hiyo kumsadia Mh.Rais kwenye ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao.
Amseyasema hayo kwenye Baraza maalum la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Boma uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Ndile ameeleza kuwa kwa Sasa Madiwani na viongozi wengine kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kwenye ukusanyaji wa mapato kwenye maeneo yao ili kuweza kufikia dhima ya Serikali juu ya uboreshwaji wa wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Niwaombe Mh.Madwani na viongozi wengine Mh.Rais wetu anafanya kazi kubwa Sana ya kutafuta pesa hivyo Basi tunapaswa kumsaidi kwenye hili ili tuweze kufikia malengo yetu" Mh.Ndile .
0 Comments