Dc Muro amesema ghala linauwezo wa kuhifadhi gunia 5,000 za alizeti sawa na tani 300 ambapo pia ghala limejengwa likiwa na vyumba vitatu vya kisasa ofisi ya chama cha ushirika, ukumbi wa mikutano ukiwa na vifaa vya kisasa vya kutolea mafunzo kwa wakulima pamoja na chumba cha kuhifadhia pembejeo za kilimo
Kukamilika kwa Ghala hili sasa kutaongeza thamani ya alizeti ambayo itatunzwa vizuri na kuuzwa katika bei ambayo itamsaidia mkulima kupata faida zaidi uku chama cha ushirika kikiwa na uwezo wa kuwahudumia wakulima wengi wanaolima alizeti katika tarafa nzima ya sepuka
Tayari Ghala limeanza kupokea mazao ya alizeti ambayo yameanza kuvunwa katika msimu huu wa kilimo, uku Dc Muro akiwashukuru wadau wa maendeleo kutoka KOICA, UNFPA, UNWOMEN, FARM AFRICA NA KIWOHEDE

Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ikungi
0 Comments