Maua Sama Awafungulia Milango Wanaume

Maua Sama ambaye ni mwanadada mwenye sauti tamu ya kumtoa nyoka pangoni kupitia nyimbo zake laini na za mahaba, amesema kuwa, jimbo lipo wazi.

Kwa, wapekuzi wa mambo jibu walilolipata kwa haraka ni kwamba, Maua Sama kwa sasa yupo tayari kufanya chaguo sahihi kwa mwanaume yeyote ambaye atavutiwa naye.
Hayo ameyabainisha Juni 27, 2022 kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo wafuasi wake wamepokea, taarifa hiyo kwa namna tofauti.

Msanii huyo wa Bongo Fleva ambaye alizaliwa Agosti 27, 1990 ameendelea kuwa na wafuasi wengi siku baada ya siku kutokana na nyimbo zake ambazo zimejikita katika ladha ya kimahaba huku zikibeba jumbe mbalimbali.

Maua Sama aligunduliwa kwa mara ya kwanza na Mwana FA mnamo 2013 baada ya kusikiliza nyimbo zake kadhaa. Mwana FA alimpeleka jijini Dar es Salaam wakashirikiana kwenye miradi kadhaa.
Miongoni mwa nyimbo zake za kwanza kuachia ni 'Mahaba Niue' ambayo aliyoitoa mwaka 2017. Toka hapo, ameendelea kutoa vibao zaidi kwa sauti yake nzuri na ya kupendeza. 
Mnamo 2018, aliachia ‘Iokote’ aliyomshirikisha msanii wa bongo Hanstone. Wimbo huu ulimpa umaarufu mkubwa sana kwa njia ambayo hakutarajia. 

Hii ilimweka kati ya majina makubwa katika tasnia ya muziki wa Tanzania. Amefanya ushirikiano na watu wengine wakubwa nchini Tanzania kama vile Harmonize na Vanessa Mdee.

Miongoni mwa nyimbo hizo ni;

1. Iokote
2. Niteke
3. Nioneshe (feat. Alikiba)
4. Mahaba Niue
5. Zai
6. Nakuelewa
7. Nioneshe
8. Main Chick
10.Wivu
11:Can Dance
12:Amen
13:This love
14:Katu Katu na nyingine nyingi. Maua Sama anasema jimbo lipo wazi, je? Haujaoa, Maua Sama anakufaa, upo tayari kukidhi vigezo vyake? Kazi kwako, wasilisha maombi upate jimbo sasa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments