Mawaziri ‘Watoro’ Waitwa Bungeni

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amewataka mawaziri waliopo bungeni kuwaita manaibu na mawaziri ambao hawapo ndani ya ukumbi wa Bunge na kwamba wanatakiwa wawepo wakati wote ambao wabunge wanajadili bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.

Akizungumza leo Alhamisi Juni 20,2022 Spika Dk Tulia amesema katika mjadala huo wa bajeti kuu ya Serikali zinajadiliwa hoja za kila wizara na kila wizara itapewa fursa ya kujibu hoja zake.

“Waheshimiwa mawaziri mliopo, naomba muwaite na mawaziri walioko Dodoma ambao hawana ruhusa ya kutokuwepo bungeni na hawajasafiri na mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) na hawajasafiri kwenda popote waje bungeni,”amesema.

Amesema bajeti kuu ni bajeti ya Serikali yote na kila mmoja anatakiwa kuchukua hoja zake zinazojadiliwa bungeni.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments