Recent-Post

Mwanafunzi Afariki Akiogelea Ziwani

Alphonce Masumbuko (17) mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari Migukulama mkoani Mwanza amefariki dunia baada ya kuzama katika Ziwa Victoria akiwa anaogelea.

Akizungumza na Mwananchi leo Juni 21, 2022 Ofisa Mtendaji Kata ya Nyanzenda, Ashura Msutu amesema tukio hilo limetokea leo saa mbili asubuhi katika kijiji cha Luchili.

Shuhuda wa tukio hilo, Joshua Atanasi amesema marehemu aliondoka na wenzake kwenda kuogelea ziwani hapo ambapo maji yalimzidi na kupoteza maisha.

Mkuu wa shule ya Sekondari Migukulama, Mashauri Lumala amekili kuwa Masumbuko alikuwa mwanafunzi katika shule hiyo aliyekuwa akisoma kidato cha kwanza.

 

Post a Comment

0 Comments