MWENGE WATEMBELEA MIRADI SITA KITETO YA BILIONI 1

Na Mwandishi wetu, Kiteto
MWENGE wa uhuru umezindua, kuweka jiwe la msingi, kukagua na kutembelea miradi sita ya maendeleo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara ya thamani ya shilingi bilioni 1.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, wrakibu mwandamizi wa Uhamiaji Mbaraka Alhaji Batenga ameyasema hayo Juni 15 wakati akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange.

Batenga mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi kwenye miradi mitatu, kuzindua miradi miwili na kupitia mradi mmoja.

Ametaja miradi hiyo ni kuweka jiwe la msingi kituo cha afya Olbolot, kuzindua mradi wa nyumba ya kulala wageni Partimbo na kuweka jiwe la msingi mradi wa maji Majengo mapya.

"Pia mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi mradi wa shule ya sekondari iliyopo Kata ya Namelok, kutembelea na kuona uendelezaji wa mradi wa zahanati ya Njiapanda na kukagua na kuzindua kikundi cha vijana," amesema Batenga.

Amesema ukiwa wilayani Kiteto mwenge wa uhuru umekimbizwa umbali wa kilomita 192 kutoka mapokezi hadi eneo la mkesha.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Sahili Nyanzabara Geraruma amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Batenga, Mkurugenzi John John Nchimbi, Mbunge Edward Ole Lekaita, madiwani, wataalam na wananchi kwa kutekeleza miradi hiyo.

Ujumbe wa mwenge wa uhuru mwaka huu ni sensa ya watu na makazi, mapambano dhidi ya rushwa, mapambano dhidi ya dawa za kulevya, mapambano dhidi ya ukimwi na kuhamasisha lishe bora kwa wananchi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments