PICHA MBALI MBALI ZA KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO ALIVYOSHIRIKI UFUNGUZI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA WA NKURUNZIZA BURUNDI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimvisha medali kapteni wa timu ya K.C.C.A ya Uganda John Revita baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya timu ya Aigle Noir FC ya Burundi na kuchukua kombe la Nkurunziza Cup, mechi hii imechezwa kwenye uwanja mpya na wa kisasa wa Nkurunziza Peace Park Complex.

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Ndugu Reverien Ndukiriyo wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex uliopo mkoani Makamba, Burundi.Vijana wa Chipukizi wa Chama cha CNDD-FDD wakionyesha burudani wakati wa ufunguzi wa uwanja mpya wa kisasa wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex uliopo katika mkoa wa Makamba nchini Burundi.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Ndugu Reverien Ndukiriyo wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja wa kisasa wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex uliopo mkoani Makamba, Burundi.Pichani baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kutoka wilaya ya Buhigwe, Kigoma wakiwa wamejumuika na wenyeji wa Burundi kama Ishara ya Ujirani mwema wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja mpya wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex uliopo Makamba nchini Burundi.Chifu Mtwale Isambe Rugali Buliho wa himaya ya Heru Juu Buha kasulu Kigoma akionyesha uzalendo kwa majirani zake wakati wa sherehe za ufunguzi wa uwanja wa michezo wa Nkurunziza Peace Park Complex, Makamba nchini Burundi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments