Rais ateua Mkuu mpya wa Majeshi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na Kumteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).

Uteuzi huo umefanyika leo Jumatano Juni 29, 2022 ambapo uapisho wa CDF Kakunda unatarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Juni 30 saa saba Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi.

Rais Samia pia amempandisha cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenereali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Wakati huohuo Rais amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF) mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo anatarajiwa kustaafu rasmi kesho, baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka saba.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments