Rais Samia Akabidhi Magari 224 Kwa TASAF Kwa Tanzania Bara Na Zanzibar

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama wakati wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi la kukabidhi magari 224 kwa Mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Tanzania Bara na Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kukabidhi magari 224 kwa Mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Tanzania Bara na Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari mfano wa Ufunguo kama ishara ya kukabidhi gari kwa ajili ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Mkoa wa Njombe katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Juni, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi wa Uratibu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bi. Siajabu Pandu mfano wa funguo kama ishara ya kukabidhi gari kwa ajili ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Juni, 2022.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama wakati akitembelea kukagua sehemu ya magari 224 kabla ya kuyakabidhi kwa Mamlaka za maeneo ya utekelezaji kwa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa Tanzania Bara na Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Juni, 2022.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments