Kwa mujibu wa taarifa iliyotelewa jana na Katibu Mtendaji wa TNBC, Dkt Godwill Wanga, maandalizi ya Mkutano huo muhimu yamekamilika na Kamati Tendaji chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussin Kattanga ilishakutana ili kuweza kujiridhisha na utekelezaji wa maazimio pamoja na maandalizi.
“Chini ya uenyekiti wa Rais Samia, Baraza limepata mafanikio makubwa katika utekeleza wa majukumu yake sambamba utekelezaji wa maazimio yake. Katika cha Kamati Tendaji wiki iliyopita wajumbe na hasa kutoka sekta binafsi wameipongeza serikali kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na uwekezaji,” alisema Dkt Wanga.
Alisema Mkutano wa Baraza utawapa nafasi wajumbe kupata taarifa za utekelezaji wa Mpango kazi wa Blue Print, Nyaraka ya Tathmini ya Mfumo wa Mapato na Matumizi ya Serikali, Tathmini ya Sekta ya Utalii na Regulatory Impact Assessment (RIA).
“Wajumbe wa TNBC wameonyesha imani yao kubwa kwa mheshimiwa Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza.
Baraza kama taasisi ni chombo muhimu kwa kuzikutanisha sekta za Umma na Binafsi pamoja na kuweza kufanya mashauriano kwa pamoja kwa manufaa na faida za kijamii na kiuchumi kwa watanzania wote.
Kuanzishwa kwa TNBC takribani miongo miwili iliyopita, mafanikio makubwa yamepatikana ikiwemo kukua kwa sekta binafsi hapa nchini sambamba na kuongezeka kwa kuaminiana kati ya sekta hizo mbili.
0 Comments