SADIO MANE KUJIUNGA BAYERN MUNICH KWA KIBUNDA KINENE

IMG-20220617-WA0119

Sadio Mane atajiunga na Bayern Munich kwa ada ya Euro milioni 41 (pauni milioni 35.2) baada ya Liverpool kukubali kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal kwa mabingwa hao wa Bundesliga. 


Mane alilengwa sana na kikosi cha Julian Nagelsmann, huku Liverpool wakikataa ofa za mapema kwa fowadi huyo, ambaye alikuwa amebakisha miezi 12 tu kumaliza mkataba wake Anfield. 


Wakati kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alipomleta nyota wa Benfica, Darwin Nunez kwa ada iliyoripotiwa kuwa ya pauni milioni 64 (€75m), pamoja na nyongeza za pauni milioni 21.4 (€25m), iliacha milango wazi kwa Mane kuondoka. 


Kocha wa Senegal Aliou Cisse alimhimiza Mane ajiunge na Bayern kama mwenye kufaa zaidi kwa maisha yake ya soka, na hatimaye klabu ya Nagelsmann imefikia makubaliano ya kukidhi pande zote. 


Stats Perform inaelewa kuwa Liverpool itapokea kitita cha uhakika cha €32million (£27.5m), pamoja na €6million (£5.2m) kulingana na mechi na €3million (£2.5m) zaidi kulingana na mafanikio yajayo ambayo Mane na Bayern watafikia. 


Ofa ya Bayern ya ufunguzi kwa Liverpool inafahamika kuwa ilikuwa €25million (£21.5m) pamoja na €5million (£4.3m) katika nyongeza ambazo zote zilihusishwa na mafanikio ya Mane na Bayern. 


Mane alifunga mabao 90 katika mechi 196 za Premier League akiwa na Liverpool baada ya kujiunga nayo akitokea Southampton mwaka 2016. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments