Sensa Ya Watu Na Makazi Kwenda Na Kuhesabu Nyumba Zote

 *Wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano wakati wa Dodoso.

Mafunzo ya waandishi wa  habari wa Mitandaoni leo yapo siku ya pili hapa mkoani Iringa huku mada kuu  ambayo imekuwa na mvuto ni uwepo wa sensa ya majengo katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itayofanyika Agosti 23 mwaka huu.  

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo Mratibu wa Dodoso la Majengo kutoka Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Amina Ramadhani amesema kuwa Sensa hii inakwenda kutambua kila jengo lililopo juu ya uso wa ardhi ya Tanzania.

"Mwaka huu kupitia Sensa ya Watu na Makazi, tunakwenda kukusanya taarifa za majengo yote nchini, tunafanya hivyo kwa kuwa hatukuwahi kuwa na taarifa hizo. Na katika hilo tumeandaa Dodoso la maswali 25" Amesema Ramadhani.

Amina Amesema lengo la sensa ya watu na makazi ni kupata taharifa sahihi za kidemografia ,kijamii,kiuchumi na hali ya mazingira kwa lengo la kupata Takwimu sahihi zitakazowezesha serikali na wadau wengine kupanga kwa usahihi mipango ya maendeleo ya watu wake katika sekta mbalimbali.

Aidha mbali na kuelezwa umuhimu wa Sensa ya majengo pia wanahabari hao wamepata kufundishwa juu ya changamoto za kuripoti habari wakati wa zoezi la sensa.

Akizungumza wakati wa kutoa mada Dkt. Darius Mukiza, Mhadhiri, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari, Chuo Kikuu Dar es Salaam amesema

bila Sensa nchi haiwezi kuweka mipango yake ya maendeleo, haiwezi kujua idadi halisi ya watu wake, kupitia sensa pia huanisha mahitaji ya huduma za jamii zinazohitajika 

 Amesema kuwa Waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii wanapaswa kuwaeleza wananchi kupitia majukwaa yao kuwa taarifa  zitakazotolewa kwa Karani wa Sensa zitakuwa Siri na zitatumika kwa madhumuni ya kitwakimu peke yake katika kusaidia serikali kupanga maendeleo.

Mratibu wa Dodoso la Majengo kutoka Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Amina Ramadhani akizungumza na Waandishi wa habari kutoka Jumikita.
Doreen Makundi ,Afisa Mipango miji  Idara ya Maendeleo ya Makazi akizunguma na Wanahabari juu ya zoezi la kuhesabu Majengo wakati wa zoezi la Sensa ya Maendeleo na makazi
Mwandishi wa Habari Pamela Molel akizungumza wakati wa mafunzo ya kuripoti habari za sensa aya watu na Makazi
Na Chalila Kibuda 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments