Serikali Imeanzisha Dirisha La Kusaidia Watoto Maskini Kupitia TASAF

SERIKALI imeanzisha dirisha maalumu chini ya mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye familia masikini ili kuendeleza kielimu na kufikia malengo yao.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema hayo wakati akisoma Bajeti Kuu ya serikali ya mwaka 2022/2023 na kuongeza kuwa, kiasi cha sh. Bilioni nane kimetengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.

Waziri Nchemba amesema dirisha hilo litakuwa chini ya Tasaf kwa sababu wao wanauzoefu na wanao mfumo kanzi data (database) ya watoto masikini wanaopatikana katika shughuli zao za kila siku.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuanzisha dirisha hilo kupitia Tasaf baada ya kuguswa na watoto wanaokatisha masomo kwa ajili ya sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kupata mahitaji muhimu.

"Licha ya kwamba serikali inagharamia elimu ya msingi hadi Sekondari bure lakini bado haitoshi, baadhi ya wanafunzi wanakatisha masomo yao kutokana na ukosedu wa kipato kutoka kwenye familia zao, mimba za utotoni, utoro, make duni wa elimu kwa baadhi ya jamii". Amesema Nchemba.

Ameongeza kuwa, pamoja na utoro, na kukabiliana na wanafunzi wanaotoka kwenye mazingira magumu, wanafunzi wengi wameshindwa kumudu mahitaji ya lazima ya shule na hivyo wabunge, madiwani na hata wasamaria kuwachangia ili kuwapunguzia ugumu wa mahitaji ya shule.

Aidha, Waziri Nchemba amesema pamoja na TASAF, pia watashirikiana na taarifa za wabunge na madiwani kutoka katika maeneo husika kupata watoto wanaotoka katika kaya maskini.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments