SERENGETI GIRLS YAFUZU KOMBE LA DUNIA KWA MARA YA KWANZA

 

Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imefuzu Michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri huo baada ya ushindi wa jumla wa mabao 5-1 dhidi ya timu ya taifa ya Cameroon katika michezo miwili iliyochezwa nyumbani na ugenini.

Serengeti Girls imefuzu Michuano hiyo baada ya mchezo wa awali kupata ushindi wa bao 4-1 nchini Cameroon, Mei 22, 2022 katika dimba la Ahmadou Ahidjo mjini Yaoundé nchini humo.

Mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye dimba la Amaan visiwani Zanzibar, Serengeti Girls imepata ushindi wa bao 1-0 pekee na kufanya jumla ya mabao 5-1 ambapo timu hiyo ya taifa ya vijana inafuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.

Michuano hiyo ya Kombe la Dunia kwa vijana wa kike itafanyika nchini India mwezi Oktoba mwaka huu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments