Dk Nchemba amesema hayo leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha hali ya uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23.
“Kati ya kiasi hicho, Sh12.8 trilioni sawa na asilimia 82.0 ya bajeti ya maendeleo ni fedha za ndani na Sh2.1 trilioni sawa na asilimia 18.0 ya bajeti ya maendeleo ni fedha za nje.” Amesema Dk Mwigulu
Amesema katika kuongeza ushiriki wa sekta binafsi kama injini muhimu ya utekelezaji wa miradi, Serikali itahakikisha miradi yote inayovutia uwekezaji wa sekta binafsi inatekelezwa kwa utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) na Joint Venture kwa kutumia utaratibu wa Kampuni Maalumu (Special Purpose Vehicle).
0 Comments