Shabiby: Serikali Mnapigwa Kwenye Magari

 

Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby amesema Serikali imekuwa ikipigwa kwenye vipuri vya magari yake kwa kununua ambavyo sio halisi (original).

Shabiby ameyasema hayo leo Jumanne Juni 21, 2022 wakati akichangia mjadala wa bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2022/2023.

Amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba kufanya uchunguzi kwenye vipuli na kwamba wamekuwa wakinunua vipuli feki.

“Nimewahi kumwambia Mbarawa (Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makeme Mbarawa) kuwa vifaa vingine mnavyonunua ni feki, mnanunua spare (vipuri) sio halisi (original) kwa hiyo mnapigwa sana,”amesema.

Aidha, ameishauri Serikali kujaribu kudhibiti na kutoa mwongozo wa magari yanayohitajika kununuliwa na viongozi.

Amesema kwa mfano wakurugenzi wanaweza wakanunua magari ya Land crusser ama double cubing.

Shabiby amesema tatizo na Serikali inataka kwenda na fashion ambapo yametoka magari mapya ya Land crusser yanayouzwa Sh500 milioni.

Mbunge huyo ameshauri viongozi wengine isipokuwa Rais, Makamu wa Rais, waziri mkuu na mawaziri watumie magari ya bei nafuu ili kupunguza matumizi kwa Serikali.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments