SIMBA SC YAMUACHA PASCAL WAWA

BAADA ya kuitumikia Simba SC kwa kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2017, Pascal Serges Wawa raia wa Ivory Coast hatoongeza mkataba na timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Simba SC imetangaza kumuacha Wawa huku ikisema atacheza mchezo wake wa mwisho siku ya Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar FC ya Mo Drrogoro ikiwa sehemu ya kumuaga Mlinzi huyo aliyedumu katika Kikosi chao kwa miaka mitano.

“Ahsante Pascal Wawa, Baada ya kutumikia timu yetu kwa misimu minne, Pascal Wawa hatakuwa sehemu ya kikosi chetu cha msimu ujao. Mkataba wake utamalizika mwisho wa mwezi huu na mchezo wa Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mchezo wake wa mwisho”, imesema Simba SC
Wawa alisajiliwa mwaka 2017 na Simba SC ikiwa ni miaka mitano sasa, awali aliwahi kuitumikia Azam FC ya Tanzania kati ya mwaka 2014-2016 kabla ya kwenda kuitumikia Al Merreikh ya Sudan kati ya mwaka 2016-2017, awali aliwahi kucheza Asec Mimosas ya nyumbani kwao Ivory Coast kati ya mwaka 2003-2010.

Katika mchezo dhidi ya KMC FC, Wekundu wa Msimbazi pia walitumia mchezo huo kumuaga Kiungo raia wa Zambia, Rally Bwalya aliyedumu katika Kikosi chao misimu miwili tangu mwaka 2020.

Post a Comment

0 Comments