SPIKA WA BUNGE AMUONYA MBUNGE WA TARIME VIJIJINI

 

Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson.

Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson ametoa onyo kali kwa Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara kwa kushindwa kutoa ushahidi wa malalamiko yake na kudharau Bunge na Spika.

Hata hivyo, ingawa Mwita amebainika kuwa anastahili adhabu kwa mujibu wa kanuni za kibunge, Spika Dk Tulia aliamua kutoa onyo na kumsamehe mbunge huyo ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Tamisemi.

Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara.

Mbunge huyo alidai Bungeni Juni 9 kuwa baadhi ya wananchi katika Jimbo lake wameuawa na Tembo na wengine kupigwa risasi na kunyanyaswa na askari wa wanyamapori. Baada ya madai hayo, Dk Tulia aliagiza serikali kufanya uchunguzi huku akimtaka Mbunge huyo kutoa ushahidi ndani ya siku nne.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments