TAIFA STARS YATOKA SARE 1-1 NA NIGER, HASIRA KUMALIZIA KWA ALGERIA

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imelazimishwa sare na timu ya Taifa ya Niger kwa kutoka 1-1 mchezo ambao ulipigwa nchini Niger.

George Mpole ndiye alieanza kupachika bao dakika 1 ya mchezo tu na kuitanguliza Taifa Stars kwa bao 1-0 kabla ya timu ya Niger kusawazisha bao kupitia kwa nyota wao Daniel Sosah dakika ya 26 ya mchezo.

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa pili kufuzu Afcon 2023 na timu ya Taifa ya Algeria, mchezo ambao utaoigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijin Dar es Salaam Jumatano hii ya Juni 8,2022.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments