VIONGOZI WA WIZARA WAKIWA BET AWARDSPicha kutoka jijini Los Angeles nchini Marekani wakati Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa alipo udhuria tamasha la utoaji tuzo za BET kwa mwaka 2022, lililofanyika usiku wa kuamkia June 27 katika ukumbi wa burudani (arena) wa Microsoft theater.

Katika ziara hiyo Waziri Mchenegerwa ameambatana na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi pamoja na Mkurugenzi wa Sanaa dkt. Emmanuel Ishengoma katika kutafuta ujuzi wa namna ya kuandaa tuzo kwa kiwango cha kimataifa, lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuitangaza Tanzania wakati ambapo Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa tuzo za MAMA – MTV African Music Awards 2023.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments