WALIOAMUA KUONDOKA NGORONGORO KWA HIYARI WAMSHUKURU RAIS SAMIA

Wakazi  wa Taarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha ambao wameamua kuhama kwa hiyari yao kwenye eneo la hifadhi wamesema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa aliouonesha kwao kwa kuhakikisha nao wanakuwa na makazi ya kudumu eneo la Msomela wilayani Handeni mkoani Tanga


Wakizungumza huku wakiwa wanaezua nyumba zao wenywe tayari kwa kuhama  wakazi kwa hiyari  wamesema walikuwa wanaisubiri fursa hiyo kwa muda mrefu lakini Rais Samia ameitekeleza, hivyo wanamshukuru sana kwa uamuzi wake.

Mkazi wa Kijiji cha Kimba wilayani Ngorongoro Beatrice  Soka amesema amefurahi sana kwasababu kwa muda mrefu walitamani mchakato huo ufanyike lakini ulichelewa.“Kwa hiyo tamko hili lilipoletwa kwa kweli mimi ni miongoni mwa watu tuliojiandikisha kwa hiyari yangu pamoja na familia yangu kwa ajili ya kwenda huko Msomela.

“Bahati nzuri nimekwenda huko Msomela na nimerudi jana.Nimeshuhudia mwenyewe kwa macho yangu na akili zangu kwa kweli fursa tuliyopewa na Rais Samia ni ya kipekee, ni ajabu, ni fursa ya upendeleo kwa wana Ngorongoro wote.

“Kuna shule, huduma ya maji , miundombinu yote na kuna mabwawa ya kutosha, nyumba, mzunguko wa nyumba kuna ekari tatu mbali na mashamba yalipo nje ya pale ekari tano na mama Samia ametuwezesha tuliotoka hapa tuweze kwenda kuendelea na kasi kwani tumepoteza muda.

Kwa upande wake 
Pasihaya Parakoi Seseka ambaye ni miongoni mwa wakazi wa Tarafa ya Ngorongoro ambaye amuamua kuhama kwa hiyari yake

Akizungumza baada ya kushuhudia zoezi hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe John Mongela amesema zoezi hilo ni la hiyari na waliyoamua kuondoka wamefikia hatua hiyo baada ya kujadilina na familia zao na kuafiki mpango huo bila kulazimishwa.


Mmoja wa Wafanyabiashara,aliekuwa akimiliki  eneo la kupumzikia Wageni (guest house) katika kijiji cha Kimba, Ngongoro  Samwel Danniel Huho akianza kuezua paa la nyumba yake akiwa ni miongoni mwa Wananchi wa kijiji hicho waliomua kuondoka  kwa hiari ili kuhama eneo hilo kupisha Uhifadhi ndani ya Ngorongoro na kuhamia katika kijiji cha Msomela, Kata ya Misima, wilayani Handeni, ambako ni makazi mapya ya wananchi wanaohamia kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mkoani Arusha.

 MKazi wa kijiji cha Kimba tarafa ya Ngorongoro ndani ya eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro katika mkoa wa Arusha,  Pasihaya Parakoi Seseka akiezua paa la nyumba yake akiwa ni miongoni mwa Wananchi wa kijiji hicho waliomua kuondoka kwa hiari kwenda kwenye kijiji cha msomela wilayani Handeni ikiwa hatua ya awali ya utekelezaji wa makubakino ya kupisha uhifadhi endelevu katika eneo hilo la urithi wa Dunia 







 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments