BILIONI 100 KUTUMIKA KUPUNGUZA MAKALI YA BEI YA MAFUTA

Naibu Waziri Wa Nishati,Wakili Stephan Byabato,Akizungumza na Wananchi Wa Wilaya Ya Siha,Mkoani Kilimanjaro,Wakati Wa Ufunguzu Wa Jengo La Maabara Katika Hosptal Kibongoto Iliyozinduliwa Na MakamuWa Rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpago Julai 16 ,2022


Makamu Wa Rais Dkt.Philip Isdor Mpago (Wa Pili Kushoto) Akisalimiana Na Naibu Waziri Wa Nishati Wakili Stephan Byabato(Wa Pili Kulia) ,Wakati Alipowasili katika Viwanja Vya Hosptal Ya Kibongoto Iliyopo Katika Wilaya Ya Siha, Mkaoni Kilimanjaro,Julai 16,2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameamua kupunguza bei ya Mafuta nchini ili kuwapatia wananchi nafuu ya maisha kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato alipokuwa akitoa salamu kwa wananchi wa Wilaya ya Siha wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Isdor Mpango inayoendelea Mkoani Kilimanjaro Julai 16, 2022.

Pia amesema bei ya mafuta duniani bado haijashuka isipokuwa serikali imeendelea kutoa ruzuku ya shilingi bilioni 100 tena kwa mwezi Julai, 2022 ili kupunguza makali ya bei ya mafuta nchini.

Bei za Mafuta zimepungua kwa takribani shilingi 270 hadi 299 kwa Mafuta ya Petroli, Dizeli imepungua kwa kiasi cha shilingi 367 hadi 460 kwa Lita Moja.

Byabato amesema kuwa, katika Wilaya ya Siha kama isingekuwa ruzuku inayotolewa na Serikali kwenye Mafuta, bei ya petroli kwa Lita moja ingekuwa inauzwa shilingi 3,539 badala ya 3,267 kwa bei ya sasa pia dizeli ingeuzwa shilingi 3,586 badala ya 3,200.

Hata hivyo, Byabato amesema kuwa Serikali imetoa shilingi bilioni mbili kwa Wizara ya Nishati ili kuwawezesha wajasiliamali wadogo wadogo kupata mikopo ya kufungua Vituo vya Mafuta katika maeneo ya Vijijini ili kufanikisha upatikanaji wa Mafuta Safi na Salama.

Ameeleza kuwa, mashariti ya kufungua Vituo vya Mafuta Vijijini yamepungua ili kuwezesha wajasiliamali kuwa na Vituo vya Mafuta.

Aidha, Byabato amesema kuwa hali ya Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro imeimalika na Umeme umewafikia Wananchi kwa zaidi ya asilimia 98 na jumla ya Vijijini 508 vimepata umeme kati ya 519, bado Vijijini 11, ambavyo vitapata Umeme kabla ya Mwaka huu kuisha.

Mkoa wa Kilimanjaro una vitongoji 2,260 kati hivyo, visivyokuwa na Umeme ni vitongoji 339 lakini hadi kufikia Juni, 2023 vitongoji vyote vitafikiwa na Umeme katika Mkoa huo.


Na. Timotheo Mathayo, Kilimanjaro.
 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments