SERIKALI MLANGONI WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA SASA NI KATA YA MANG'ONYI

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Nd. Jerry C. Muro ameendelea na ziara ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na safari hii ni katika kata ya Mang'onyi kijiji cha Mang'onyi

Kati ya kero kubwa iliyokuwa inalalamikiwa na wananchi ni utendaji kazi wa mwenyekiti wa kijiji Issa ahmed almas ambae wananchi wamesema ameshindwa kuwasikiliza na kutatua kero zao uku akiendelea kufanya matumizi mabaya ya fedha za kijiji hatua ambayo imewafanya wamkate mbele ya Dc Muro

Kutokana na changamoto hiyo Dc Muro alilazimika kusimamia mchakato wa kiutaratibu wa kisheria na kikanuni wa kumuondoa mwenyekiti huyo ambapo mkutano mkuu wa kijiji ulipiga kura ya kumkataa mwenyekiti hatua jambo lililopelekea wananchi kupendekeza majina ya wananchi wawili ambao walipigiwa kura ya kukaimu uenyekiti wa kijiji na nafasi kuchukuliwa na Elineema Sethi mtinangi ambae ni mwenyekiti wa kitongoji cha Mang'onyi stendi
Mara baada ya mabadiliko hayo Dc Muro alianza kutatua kero ya changamoto ya maji kwa kuagiza wataalamu wa Ruwasa kufika kijijini na kurekebisha kisima cha taru milimani ili wananchi wapate maji

Changamoto ya pili kwa wananchi wa Mang'onyi ni hofu ya kukumbwa na baa la njaa kutokana na kukosekana kwa mvua za kutosha katika kilimo huenda zikasababisha njaa na Dc Muro kuagiza tathmini ya hali ya athari za kilimo katika msimu huu ianze katika ngazi ya kijiji na kubaini kaya ambazo zitakuwa na upungufu wa chakula ili zianze kutafutiwa msaada wa chakula haraka.

Tazama Picha Mbali Mbali Za Matukio   Hapa                     

                   

Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ikungi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments