CCM Kujadili Mfumuko Wa Bei

Kutokana na mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali nchini, Makamu Mwenyekiti was Chama Cha Mapinduzi CCM, Abdulrahman  Kinana amesema Chama hicho kimejipanga kufanya kikao mwezi ujao kujadili suala hilo.

Kinana amebainisha hayo leo Julai 28, 2022 baada ya kupokewa na wakazi wa Mkoa wa Mbeya wakati akitokea Mbozi mkoani Songwe.

Msingi wa kueleza hayo ni baada ya wananchi waliojitokeza kumpokea kunyoosha mabango na wengine wakiongea wakidai hali ya maisha yao kwa sasa ni magumu kutokana na bidhaa nyingi kupanda bei kupanda madukani.

"Mfumuko wa bei nakubaliana nanyi, tutakuwa na kikao cha NEC mwezi ujao na moja ya mambo ambayo yataangaliwa kwa kina na umakini ni mfumuko wa bei kuona tunafanya nini Ili bidhaa zishuke bei kupunguza ukali wa ugumu wa maisha,"amesema Kinana

Simoni Mwambene amesema ugumu umeongezeka zaidi vitu walivyokuwa wananuanua kwa Sh500 sasa vimepanda hadi Sh1000.

"Tukianza na mahitaji madogomadogo yamepanda bei madukani sabuni za kuogea tulikuwa tunanunua Hadi sh 500 sahizi imepanda hadi sh 1000 inaumiza hasa kwa sisi wenye familia alafu vipato vyetu ni vya chini,"amesema

Maria Mwakifula amesema viongozi waangalie namna ya kudhibiti mdumuko wa bei ya bidhaa kwani wanaoumia ni Wananchi wa chini.

"Ukiachiwa Sh10000 kwa ajili ya matumizi ya ndani haitoshelezi tunawaomba viongozi watusaidie kutatua changamoto hii kila kukicha bei zinapanda,"amesema

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments