CHONGOLO AKEMEA WANAOSAKA UBUNGE SASA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akizungunza KATIKA mkutano wa Katibu Mkuu Chongolo ameyasema hayo leo tarehe 13 Julai, 2022 wakati akifungua kongamano la Mafunzo ya Uongozi kwa mabalozi wa mashina na viongozi wa matawi mkoa wa Dodoma .


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya wanachama kuanza kujipitisha katika majimbo kutafuta wapambe ili wawasaidia kwenye malengo yao ya Ubunge na udiwani kwa mwaka 2025.

Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Chama hakitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa taratibu, kanuni na katiba ya CCM ili kuwadhibiti watu hao, kwani muda wa uchaguzi bado na sasa kila jimbo lina mbunge na kila kata kuna diwani hivyo ni vema kwa kila mwanachama kusubiri muda ufike na sio kuanza sasa wakati viongozi waliochaguliwa wanafanya kazi ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.

Katibu Mkuu Chongolo ameyasema hayo leo tarehe 13 Julai, 2022 wakati akifungua kongamano la Mafunzo ya Uongozi kwa mabalozi wa mashina na viongozi wa matawi mkoa wa Dodoma .

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments