Gari la Royal Tour latinga Sabasaba

Gari aliyoendesha Rais Samia Suluhu Hassan wakati akirekodi filamu ya The Royal Tour limetinga katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 maarufu Sabasaba na kugeuka kivutio.

Gari hiyo liliyowasili saa 5 asubuhi lilikuwa likisindikizwa na magari mengine sita huku likitembea mwendo wa polepole ndani ya uwanja huo.

Kabla ya kuegeshwa katika banda la Maliasili na Utalii kwa ajili ya watu kuliona kama kivutio sehemu zote ambazo gari hilo lilipita lilikuwa kivution.

Hiyo ni kutokana na askari 12 kulilinda gari hiyo ambao walikuwa wakitembea kwa mwendo wa kunyata huku wakiwa sita kila upande.

Pia ujio wa gari hilo ulipambwa na kikundi cha ngoma kilichokuwa kimetangulia mbele jambo ambalo lilifanya waliohudhuria katika maonyesho hayo kuangalia huku wengine wakishangaa.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Felix John amesema wameamua kuleta gari hilo katika maonyesho ya Sabasaba ili watu waweze kuliona na watakaohitaji wapige picha nalo.

"Lakini gari hii ni la muhimu na litaendelea kuwepo vizazi na vizazi waweze kuliona"

Filamu hii iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza Aprili 18 mwaka huu nchini Marekani irekodiwa ili kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini huku ikilenga kuongea idadi ya waatalii na wawekezaji nchini.

Rais Samia alianza kurekodi filamu hiyo Agosti 29, 2021 kwa lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia vivutio vya utalii.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments