HAJI MANARA AFUNGIWA MIAKA MIWILI NA FAINI YA MILIONI 20

Msemaji  wa Yanga SC, Haji Manara amefungiwa kujihusisha na masuala ya Soka ndani na nje ya nchi baada ya kukutwa na makosa ya kumtishia, kumdhalilisha Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kuchafua sifa, taswira ya Soka la Tanzania kwa ujumla.

Akisoma hukumu hiyo mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho hilo, Walter Lungu amesema Kamati hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya kupokea malalamiko hayo kutoka Sekretarieti ya Maadili ya TFF.

Lungu amedai shitaka la kwanza Mlalamikiwa anadaiwa kusema maneno dhidi ya Rais wa TFF kwenye mchezo wa Fainali ya ASFC, “Wewe unanifuata fuata sana na hii mara ya tatu, sikuogopi kwa lolote, nina uwezo kukufanya chochote na huna uwezo wa kunifanya lolote”.

Licha ya Mlalamikiwa kuomba radhi kwa Rais wa TFF, Wadau, Mashabiki wa Soka na Waandishi wa Habari, Lungu amesema hukumu hiyo imetolewa chini ya Kifungu cha 73 (5) na (6) vya Kanuni za Maadili ya TFF, Toleo la 2021, huku akitoa taarifa ya rufaa kwa pande zote mbili.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments