KATAVI KUUNGANISHWA NA GRIDI YA TAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, ameagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha ujenzi wa Kituo cha kupoza Umeme wa Gridi ya Taifa cha Inyoga kukamilika ifakapo Oktoba 2023.

Makamu wa Rais yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya kiserikali kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo Kituo cha kupoza umeme cha Inyonga, Julai 21, 2022.

Akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Mlela, Mkoa wa Katavi, kata ya Inyoga alisema kuwa haridhishwi na kasi ya Ujenzi wa kituo cha kupoza Umeme cha Inyonga kinachotegemea kuzalisha megawati 12.

Dkt. Mpango aliagiza ujenzi wa vituo vya kupoza Umeme vya Ipole na Mpanda Mjini unakamilishwa haraka pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Katavi yenye urefu wa kilomita 383.

Alisema kuwa fedha za kulipa fidia ili kupisha Ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme kutoka Tabora hadi Mpanda zimeshatolewa na Serikali, hivyo uthamini wa mali za Wananchi watakaoathirika na ujenzi wa njia hiyo ufanyike ili walipwe na mradi uanze kutekelezwa.

Ameagiza shirika la Umeme nchini (TANESCO) kupitia Wizara ya Nishati kupeleka mashine ya kuzalisha Umeme kutoka Wilaya ya Loliondo ifikapo mwezi Oktoba, 2022 ili kuongeza uzalishaji wa umeme katika Mkoa wa Katavi.

kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akitoa salamu za Wizara kwa Wananchi wa Wilaya ya Mlela alisema Mkoa wa Katavi una Vijiji 52 ambavyo havijapata umeme kati ya Vijiji 152 vilivyopo.

Alisema vifaa mbambali kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya kuzalisha Umeme katika Mkoa wa Katavi kama nguzo, mashine umba pamoja na waya vipo tayari, hivyo kufikia mwezi Oktoba 2023 mradi wa kupeleka Umeme katika Vijiji vilivyobakia utakuwa umekamilika.

Aidha Ameeleza Kuwa  baada ya hatua hiyo, Wizara kupitia Taasisi zake zinazoshughulika na masuala ya Umeme, zitaanza utekelezaji katika ngazi za vitongoji ili kuhakikisha umeme unamfikia kila mwananchi bila kujali umbali uliopo.

Kuhusu suala la Uzalishaji umeme katika Mkoa wa Katavi, alisema kuwa Wizara inaendelea na usimamizi wa ujenzi wa vituo vitatu vya kupoza Umeme ambavyo ni Inyoga, Mpanda Mjini pamoja na Ipole vitakavyozalisha jumla ya megawati 32 pindi vitakapokamilika.

Mkoa wa Katavi unapata umeme kupitia chanzo cha jenereta ingawa jitihada za kuhakikisha mkoa wa unapata umeme wa  uhakika kabla kuunganishwa na gridi ya taifa zinaendelea ikiwemo kuleta mashine ya umeme kutoka loliondo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 1.25 kabla ya octoba 2022 zinaendelea.

Kwa Upande Wa Naibu Waziri Wa Nishati Byabato AliseMa  kuwa  Kapuni tanzu ya TANESCO ya ETDCD inaendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye urefu wa kilometa 383 kutoka Tabora mjini kwenda Ipole,Inyoga hadi Impanda Mjini yenye msongo wa kilovoti 132 ambapo jumla ya sh.bilioni 148 zimetolewa kwajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Aidha ameeleza kuwa jumla ya sh.bilioni 500 zimetolewa na serikali ili kuhakikisha maboresho yanafanyika kwa kujenga vituo vya kupoza umeme nchini pamoja na shughuli za usambazaji umeme kwa lengo la kuimalisha gridi ya taifa

Na Timotheo Mathayo, Katavi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments