KENANI KIHONGOSI AWASIHI VIJANA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA....AANIKA MAFANIKIO LUKUKI

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndugu Kenani Kihongosi amewataka Vijana kumuunga mkono Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.


Ameyasema hayo leo Julai 3,2022 alipokuwa anahutubia katika Mahafali ya UVCCM Seneti ya Dar es salaam Tarehe 03 Julai 2022.


"Wajibu wetu mkubwa Vijana ni kusimama na Serikali, kusimama na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kusimamia na Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, matunda ya miradi hii ya kimkakati wanufaika wakubwa ni sisi vijana na watoto wetu kwa miaka mingi baadae"


Ndugu Kenani Kihongosi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika Taifa letu ya kuhakikisha Vijana wanapata ajira pamoja na kuendeleza Miradi Mikubwa ya kimakakati.


"Tunampongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyenkiti wetu wa Chama cha Mapinduzi, ninyi wenyewe ni mashahidi miaka sita nyuma hapakua na ajira kwenye utumishi wa umma lakini yeye ndani ya mwaka Mmoja Mhe Rais ametoa ajira zaidi ya elfu 79 Watumishi wa umma tunampongeza sana".


"Tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa kutoa ajira, nyinyi wenyewe ni mashahidi takriban miaka sita Serikali haikuajiri watumishi wa Umma, ndani ya mwaka mmoja wa Mhe Rais Samia ametoa Ajira zaidi ya elfu 76"


"Mhe. Rais Samia, ameendelea kufanya kazi kubwa, miradi ya kimkakati inaendelea Ujenzi wa bwawa la kufua Umeme la Mwalimu Nyerere linalogharimu zaidi ya Trilioni 6 ambalo litazalisha Umeme Megawatt 2115, ujenzi umefikiaikia asilimia 62 kutoka asilimia 41 alipoupokea Mhe. Rais Samia"


"Tunao mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) hadi kufikia Aprili 2022, ujenzi wa Reli kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (km 300) umefikia asilimia 96.54 na kipande cha Morogoro - Makutupora (km 422) umefikia asilimia 85.02 na tumeona treni ya majaribio ipo katika majaribio Kazi Inaendelea"


Lakini pia katibu Mkuu ameeleza kuwa Vijana wana kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufuta ada kuanzia kidato Shule za Msingi hadi selondari kwani kufutwa kwa ada kunaenda kuleta nafuu kubwa kwa Familia nyingi Tanzania na kihakikisha Vijana wote wanapata Elimu Bora.


" Wengi tunajua adha ya kitu kinaitwa Ada, Tunampongeza Mhe. Rais Samia kwa kufuta Ada ya kidato cha Tano na cha Sita, jambo hili ni kubwa linakwenda kuwasaidia Watanzania walio wengi kupata Elimu bora"


Pia Katibu Mkuu UVCCM Taifa amewataka Vijana Kuhasiaha Kuhusu Sensa na kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi Kuhesabiwa kwani Sensa ni msingi wa maendeleo katika Taifa.


" Vijana twendeni tukahamasishe Sensa na tukawaambie Sensa ndio msingi wa Maendeleo kwa katika nchi yatu, bila kujua idadi ya watu Serikali haiwezi kufanya Maendeleo yanayotakiwa, niwaombe sana tumuunge mkono Mhe Rais Samia na Serikali yetu kuhakikisha tunakuwa Mabalozi wema wa kuhamasisha Sensa"


Kuhusu Kilimo Katibu Mkuu ameeleza ni kwa kiasi gani Mhe Rais Samia Suluhu Hassan anajua umuhimu wa Kilimo katika Taifa Letu kwani uwekezaji wa Fedja nyingi katika kilimo inaonyesha maono yake makubwa aliyoyabeba kwa watanzania.


"Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, katika Sekta ya Kilimo ameongeza Bajeti kutoka Bilioni 294 hadi Bilioni 900 haijawai kutokea katika historia ya Taifa hili akitambua kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu, tumejionea maafisa ugani nchini nzima wamepewa vifaa mbalimbali ili kuiboresha Sekta ya Kilimo"


Mwisho Katibu Mkuu Ndugu; Kenani Kihongosi amesema kuna watu walinnzani mambo yatakwama lakini wamekwama wao maana Kazi inaendelea na hakuna mradi hata mmoja uliosimama Tangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan aingie Madarakani. "Kuna watu walizani kuna mambo yatasimama hatimae wamesimama wao Mama anaendelea kuupiga mwingi, wajibu wetu Vijana ni kumuunga mkono Mhe. Rais Samia na kumsemea na kumwambi Mama Ulipo Tupo Kama Vijana


#AlipoMamaVijanaTupo
#2022ShirikiUchaguziKwaUadilifu
#2022JiandaeKuhesabiwa
#KaziIendelee

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments