KIDUNDA BINGWA WA WBF AMCHAPA KATOMPA .

Bondia Mtanzania, Kutoka JWTZ Seleman Kidunda amefanikiwa kumchapa kwa ushindi wa majaji wote watatu mpinzani wake kutoka DR Congo, Tshimanga Katompa katika pambano la ubingwa wa WBF lililofanyika uwanja wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma.


Akizungumza Mara baada ya kushuka ulingoni Seleman Kidunda amewashukuru watanzania na mashabiki wa ngumi kwa sapoti yao licha ya Mpinzani wake kuwa bondia mzuri amehakikisha anaibuka na Ushindi katika ardhi ya nyumba kwao.

Kwa upande wa bondia Erick Katompa Amesema,mchezo ulikuwa mzuri licha ya kupoteza Pambano hilo dhidi ya mpinzani wake Kidunda.

Huku Bondia Mwenye Mikwara Mingi Karimu Mandonga akipata kipigo cha TKO Kutoka kwa Shabani Kaonekana raundi ya tatu.

Mabondia Wengine walioshinda Ismail Galiano akimtwanga KO, Buda Chikoko kutoka Malawi, George Bonabucha akimtandika kwa TKO, Yusuph Alli,Ezra Paul amefanikiwa kumchpa kwa KO ya raundi ya kwanza, Kasim Gambo, Grace Mwakamele amemtandika Suzana Mahenge kwa TKO, Khalid Chokoraa ameambulia sare dhidi ya Chidi Benga huku Musa Chitepete akimchapa Salvatory Urio kwa pointi.

Licha ya Mpinzani wake kuwa bondia mzuri amehakikisha anaibuka na Ushindi katika ardhi ya nyumba ili kuendelea kuupa heshima mchezo wa ngumi ni Tanzania.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments