KINANA ASEMA RAIS SAMIA ANAZUNGUMZA POLEPOLE LAKINI VITENDO VINGI.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amemmwagia sifa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa anayofanya ya kuleta maendeleo ya Watanzania.

Kanali Mstaafu Kinana ametoa sifa hizo kwa Rais Samia wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika Mkoa Mbeya.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa maeneo mbalimbali nchini na kwamba amekuwa ni kiongozi anayezungumza polepole lakini vitendo vyake ni vingi kwani kila mkoa , kila sekta kuna fedha nyingi za maendeleo.

“Kote ambako nimepita tangu nilipoanza ziara mkoani Katavi na baadae Rukwa , Songe Rais Samia amepeleka fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo na hapa Mbeya Mkuu wa Mkoa ametoa ushahidi wa fedha nyingi zilizotolewa na Rais kwa ajili ya miradi ya maendeleo,”amesema Kinana

Aidha Kinana amewapa salamu za Rais kwa wananchi hao kwamba atafika katika mkoa huo kwenye Maonesho ya Wakulima Nane yatakayofanyika kitaifa katika mkoa huo na kabla ya Rais Samia Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango naye atakwenda katika mkoa huo.

“Mkoa wa Mbeya umepewa hadhi ya aina yake na ndio maana mmekuwa mkipokea wageni wengi na Rais Samia amenip salamu zenu kuwa atakuja hapa kuhudhuria maonesho ya Nane Nane.

Kuhusu changamoto ambazo menipatia nitampelekea Rais,”amesema Kinana.Pamoja na salamu hizo Kinana amesisitiza Rais Samia anajituma anatafuta hela kwa njia mbalimbali  na wananchi wakiwemo wa mkoa wa Mbeya wamekuwa mashuda.“Tangu Rais ameingia madarakani kuna fedha zinatolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

”Katika hatua nyingine Kinana amezungumzia umuhimu wa reli ya TAZARA kwa wananchi wa mkoa huo katika kusafirisha abiria na mizigo na kwamba Serikali ya China iko tayari kuikarabati na Rais Samia yuko tayari kuisimamia ukarabati huo.

Amesema reli ya TAZARA mbali ya kuwa kichocheo muhimu cha kukuza uchumi wa wananchi pia imekuwa kiunganishi kikubwa kati ya nchi za Tanzania na Zambia.“Tukiimarisha reli hii tutakuwa na usafiri wa uhakika”.

Aidha amewapongeza viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM na Serikali kwa namna wanavyoshiriki kikamilifu kusimamia maendeleo ya maeneo yao.

“Mmesikia miradi ya maendeleo, wabunge wanafanya kazi nyingi bungeni.“Wakati mwingine wanafanya kazi nje ya Bunge, wanakwenda kuzungumza na mawaziri na manaibu waziri kwa ajili ya kutafuta fedha,”amesema Kinana.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homela amemueleza Kinana kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa ya maendeleo ndani ya mkoa  huo na sasa anakwenda kutatua tatizo sugu la barabara ambayo imekuwa kilio cha muda mrefu ambapo ujenzi wa barabara wa njia nne unatarajia kuanza na fedha zimeshapatkana.

“Kwanza kabisa yako mambo anayofanya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan , hapa Mbeya kwenye upande wa maji ametekeleza miradi mingi.

“Kubwa kuliko mradi wa maji unaokwenda kutoa lita milioni 300 kupitia chanzo cha mto Kiwira ambao unakwenda kuondoa changamoto ya maji mkoa wote wa Mbeya.Pili Rais ametujengea jengo la mama na mtoto ambalo sasa limekuwa kivutio cha utalii.

“Jengo hilo alilianza Rais John Magufuli na juzi tumepata Sh.bilioni mbili na ujenzi umefikia asilimia 97 na jengo litakuwa linahudumia akina mama 400 waliojifungua kwa wakati mmoja.

Pia Rais Samia ametuweka taa za Sh.bilioni 32 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe,”amesema Homela wakati anaelezea maendeleo ya mkoa huo.

Amefafanua kwa maendeleo ambayo Rais Samia ameyapeleka katika mkoa huo wana kauli mbiu inayosema Rais Samia Mbeya ni yako na majibu yako 2025 .

Wakati nyingine inasema Samia ameshaupiga mwingi, goli liko nyavuni , hivyo wanasubiri kushangilia 2025.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments