KINANA: VIJANA, WANAWAKE JITOKEZENI UCHAGUZI NDANI YA CCM TUTATENDA HAKI.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana akizungumza na wananchi na wana CCM wa jimbo la Nsimbo mkoani Katavi baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Itenka leo Julai 25,2022 .

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM - Bara), Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mlindoko, pamoja na viongozi wengine Chama wa Mkoa huo baada ya kuwasili mkoani humo jana. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
Kanali Mstaafu Kinana akiweka jiwe la Msingi la Kituo Cha Afya Itenka
Akishiriki ujenzi wa kituo hicho Cha afya.

Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na wana CCM na wananchi baada ya kuweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya Itenka.

kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na wana CCM na wananchi baada ya kuweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya Itenka.
(Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
MPANDA
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM-Bara), Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amewataka wanawake na vijana nchini kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi za ungozi ndani ya Chama na kuwahakikishia kuwa haki itatendeka huku akisema hakuna wa kumtisha mwenzake.

Kinana ameyasema hayo mjini Mpanda mkoani Katavi, wakati akizindua mradi wa fremu 15 za maduka zilizojengwa katika Ofisi za CCM za mkoani humo, ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia uchaguzi unaoendelea ndani ya CCM.

Akifafanua zaidi Kinana alisema, uchaguzi ndani ya Chama upo katika hatua mbalimbali hivyo ni vyema wana CCM wakajitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili kuwania nafasi za uongozi.

"Niwaombe akina mama mkachukue fomu msiogope, nendeni mkachue fomu mpambane na wanaume.

"Nataka niwasihi vijana gombeeni hizo nafasi, uchaguzi ukija nafasi zitakuwa wazi na kila mtu anahaki sawa na mwenzake, hakuna masultani wa kukaa madarakani milele, tuna uchaguzi kila baada ya miaka mitano, wenye kuwachagua viongozi ni wana CCM, wakikupenda, wakikuheshimu na wakithamini mchango wako watakupa kura, wasipothamini watakunyima kura.

"Nafikiri na ninyi mnawafahamu wajumbe sio watu wazuri, wanaweza kukwambia usiwe na wasiwasi tutakupa kura, halafu baadae unatoka kapa, hivyo niwaombe sana vijana gombeeni, kina mama gombeeni, tutatenda haki, hatutampendelea mtu, wala mtu asimtishe mwenzake, kwamba ukienda kuchukua fomu unaambiwa na wewe unatafuta nini, kwani na wewe ulivyochukua fomu mwingine sialikuwepo kabla yako, ndio umechukua nafasi yake na mimi nakuja kukung'oa wewe," alisema.

Kanali alisema Chama kitazingatia demokrasia na hakitampendelea yeyote katika uchaguzi huo ili kuwapata viongozi wenye kukubalika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments