KINANA:SEKTA BINAFSI INAANZA NA WANANCHI WA KAWAIDA

 Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana amewataka viongozi na watendaji wa serikali kuhakikisha wanarahisisha ufanyaji wa shughuli za wananchi kwa kuwaondolea vikwazo kwa kuwa sekta binafsi inaanza na wao.


Kinana ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Nkasi Kaskazini eneo la Lyazumbi wakati wa mapokezi ya kuanza ziara mkoani Rukwa akitokea mkoa wa Katavi.

"Serikali inafanya jitihada za kuimarisha na kuboresha mazingira ya sekta binafsi nchini ili ifanye vizuri, sasa sekta binafsi inaanza na wananchi wa kawaida. Tuwaondolee kero wananchi wetu na tuwarahisishie kufanya shughuli zao iwe ni wakulima, wafugaji, bodaboda, wamachinga au wafanyabishara." Amesema Kinana

Akimkaribisha mkoani Rukwa Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Ndugu Rainer Lukalah
amemueleza Ndg Kinana kuwa hali ya siasa katika mkoa huo ni shwari na wanaridhishwa na kazi kubwa ya maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kinana ameingia mkoani Rukwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya uimarishaji chama na ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa jimbo la Nkasi (hawapo pichani) wilayani Nkasi mkoani Rukwa baada ya kuwasili akitokea mkoani Katavi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments