MATUKIO MBALIMBALI BANDA LA WIZARA YA FEDHA SABASABA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo (Kushoto) akiongea na Mstaafu Bi Sura Rwiza (kulia) aliyefika kuhakikiwa katika Banda la Wizara kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade), Jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja. 

Mkurugenzi wa SELF MICROFINANCE, Bw. Mudith Cheyo, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Tehama Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Zuberi Msisi, kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar Es Salaam (TanTrade), Jijini Dar Es Salaam 

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Pro. Eliamani Sedoyeka (Kulia) akifurahia jambo baada ya kupata Elimu kutoka kwa maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade), Jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja 

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Pro. Eliamani Sedoyeka (Kulia) akipokea machapisho kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bi. Shamimu Mdee, kwenye Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade), Jijini Dar Es Salaam 

Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar Es Salaam (TanTrade),kushoto ni Afisa Mapokezi na Katibu Muhtasi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Masia MsuyaNaibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo (aliyeshika tuzo) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) ambacho kimeibuka mshindi wa tatu katika tuzo ya jumla kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu vinavyoshiriki Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Tantrade). Kutoka kulia ni Afisa Uhusiano wa Chuo hicho Bi Sarah Goroi, Afisa Uhusiano Bw. Anold Kavishe na kushoto ni Afisa Masoko Benadetha Inyasi

Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Takwimu Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka kulia ni Bi Neema Madembwe Kushoto kwake ni Afisa Maktaba Mkuu Bi Mwanaabu Ngulumbi alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade), Jijini Dar Es SalaamNaibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akizungumza na Afisa Udahili wa Chuo cha Mipango ya maendeleo Vijijini (IRDP) Dkt Maclean Mwamlangala (Kushoto) kulia ni Afisa na Uhusiano Bi Stellah Masanja alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es Salaam (TanTrade) Jijini Dar Es Salaam

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango- Dar es Salaam)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments