MBUNGE CCM AMTWISHA KINANA KERO YA UWANJA WA NDEGE MKOANI RUKWA

Mbunge  wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hilaly amemueleza Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana kwamba ombi kubwa la wananchi wa Sumbawanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla ni kuwa na uwanja wa ndege.


Akizungumza kwenye kikao cha ndani kilichohusisha wanachama wa CCM Mkoa wa Rukwa, Mbunge Hilaly amesema kuwa wanashukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuleta maendeleo katika Nyanja mbalimbali.

“Wananchi wa Sumbawanga na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla tumeendelea kushuhudia maendeleo makubwa yakifanyika, miradi ya maendeleo imeendelea kutekelezwa.Katika bajeti ya mwaka huu tumepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami kilometa 21 ambazo zitajengwa Sumbawanga Mjini.

‘Vijiji vyetu vyote vitapata maji, nawaomba niwahakikishie Sumbawambawanga tuko salam, tuko vizuri.Kwa mambo ambayo yamefanyika Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara tunakuhakikishia kura za mwaka 2025 tutazilinda kwa gharama zote,”amesema Hilaly.

Aidha amesema kuwa wabunge wamekuwa wakifanya ziara mbalimbali kuelezea wananchi yale ambayo wameyafanya na wanayokusudia kuyafanya katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Pamoja na hayo Mbunge huyo amesema kwamba kero yao kubwa kwa sasa ni uwanja wa ndege hivyo wametoa ombi kwa Makamu Mwenyekiti achukue kero hiyo na kuifikisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili nao wawe na uwanja wa ndege.

“Inawezekana wote tusipande ndege lakini uwanja ukijengwa tutapata wageni wengi na hivyo wapo watakaokuja kuwekeza na kufungua milango ya maendeleo.Tunafahamu katika ujenzi wa barabara hatuna tatizo, tunazo barabara za kutosha na nyingine zinaendelea kujengwa.Hivyo kero yetu ni uwanja wa ndege.

“Tulipokuwa kwenye Bunge la Bajeti tuliomba uwanja wa ndege lakini tunaamini kupitia Makamu Mwenyekiti wa Chama chetu ukituombea tutapata uwanja utakuwa umetuongezea nguvu,”amesema Mbunge huyo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana akifafanua jambo kwenye kikao cha ndani cha Viongozi Waandamizi wa CCM mkoa baada ya kupokea taarifa mbalimbali ikiwemo na baadhi ya changamoto zilizomo ndani ya mkoa huo namna ya kuzitafutia ufumbuzi na hatimaye kuwaondolea Wananchi Kero
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe Joseph Mkirikiti alipokuwa akieleza baadhi ya changamoto zilizopo ndani ya mkoa wake na namna ya kuzitafutia ufumbuzi na hatimaye kuwaondolea Wananchi Kero
MBUNGE wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hilaly akimueleza Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana kuhusu kero yao kubwa kwa sasa ambayo ni uwanja wa ndege na kutoa ombi kwa Makamu Mwenyekiti achukue kero hiyo na kuifikisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili nao wawe na uwanja wa ndege.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments