Mbunge Fredrick Lowassa Afanya Jambo Soko Kuu la Monduli

 Mbunge wa Jimbo la Monduli wilayani Monduli Mkoa wa Arusha, Fredrick Lowassa ametoa shilingi millioni 3.8 kwa ajili ya ukarabati wa paa la Soko Kuu la Monduli. 

Hayo yalijiri wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya maendeleo ikiwemo barabara ya Monduli mjini inayojengwa kwa Kiwango cha lami ambapo wakati wa ukaguzi huo alisimamishwa na wafanyabiashara wa soko hilo na kutoa changamoto zao ikiwemo uchakavu wa soko hilo, na maji kujaaa ndani ya soko kipindi cha mvua.

Awali akizungumza mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo ambaye hakutaka kutajwa majina yake amesema changamoto yao kubwa ni miundombinu ya soko hilo, pamoja na kuomba kuondolewa kwa soko moja kwani wamekuwa wakimwaga vitu kutokana na kuharibika, kwani masoko yamekuwa mengi maarufu kama magulio.

Josephat Mbilinyi ni mwenyekiti wa soko hilo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo pamoja na ukosefu wa mikopo zile asilimia kutoka halmashauri kwenda kwa wajasiriamali. 

Pia Mbunge Lowasa ametoa ahadi ya pikipiki 12 ambazo zitatolewa wiki ili ziweze kunufaisha kila kijiwe kilichopo Monduli Mjini.

Chanzo diramakini

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments