Mbunge Wa Viti Maalum Husna Sekiboko Agawa Vifaa Vya Ofisi Zote Za UWT Tanga Vyenye Thamani Ya Milion 14

Mbunge wa Viti Maalum Tanga, Husna Sekiboko amesisitiza umuhimu wa

Chama Tawala na Jumuiya zake (Umoja wa Wanawake), Wazazi na Umoja wa
Vijana) kufanya shughuli zao kuendana na matakwa ya teknolojia ya
kisasa.

Sekiboko amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa kompyuta
13 za mezani, printa na vifaa vingine, rimu za karatasi vyote vikiwa
na thamani ya zaidi ya Sh milioni 19 zilizotolewa na wabunge watatu wa
Viti Maalumu kwa ajili ya ofisi za UWT katika wilaya tisa na matawi
mengine ya chama tawala.

Sekiboko alitoa kompyuta 10 ,rimu na Printer zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 14
Mbunge mwingine, Mwanaisha Ulenge
ametoa kompyuta tatu na rimu zenye thamani ya Sh zipatazo million
5 huku Mwantumu zodo akitoa rimu katoni 20.

Sekiboko amesema kuwa shughuli za kisasa zinahitaji teknolojia ya
kisasa na amesema ndiyo maana wamekubali ombi la kusaidia uendeshaji
wa ofisi kuwa za kisasa lililofanywa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa
Tanga, Dk Aisha Kigoda.

"Ni jukumu letu kama wanachama na viongozi wa CCM kusaidia kujenga
chama na kuzibadilish kuwa taasisi za kisasa za chama inayofanya kazi
kwa kutumia mapinduzi ya kidijitali," Sekiboko amesema.

Akipokea kompyuta hizo, Mwenyekiti wa UWT Mkoa, Dk Aisha Kigoda
aliwashukuru wabunge hao wa Viti Maalum waliochaguliwa kupitia UWT
kutumia vifaa hivyo vya kisasa ili kuboresha utendaji kazi wa Umoja
huo.

Aidha aliwataka Makatibu wa UWT wa Wilaya na menejimenti kutumia vifaa
hivyo vya kisasa kutengeneza mapendekezo ya mradi ili kuwezesha jumui
hiyo kujitegemea.

“Changamoto yetu kubwa kwa sasa ni ukosefu wa miradi ambayo
ingewetuzesha kujitegemea. Jumuiya zote za Chama zimeelekezwa kujenga
nyumba za watumishi na wilaya zote kwa sasa ziko katika hatua tofauti
za utekelezaji wa agizo hilo,” amesema.

Amesema hivi sasa baadhi ya wilaya zipo katika harakati za kupata
viwanja au kutafuta hati miliki lakini Muheza wapo mbele sana na kwa
sasa wanaendelea na ujenzi wa msingi.

Kigoda amesema kuwa uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi ndio jibu
pekee la kuweza kufadhili miradi yetu.

"Lazima tujitahidi kuunda miradi ambayo itatufanya kujitegemea," amesema.

Dk Kigoda pia alizitaka Ofisi za UWT kutumia vifaa vya kisasa vya
kuhifadhi taarifa hizo ikiwa ni pamoja na idadi ya wanawake na vikundi
ambavyo tayari vimepata mikopo kutoka vyanzo mbalimbali na kufuatilia
ili kuona iwapo mikopo hiyo imekuwa na athari katika ustawi wao
kiuchumi.

Awali Katibu wa UWT Mkoa wa Tanga, Aziza Hussein Kiduda amesema
kompyuta na printa hizo zitaboresha utendaji wa kazi zao.

Amesema kuwa Mbunge wa Viti Maalum Husna Sekiboko amekubali kusaidia
mafunzo ili kuwawezesha watumishi wa UWT kutumia kompyuta kwa ufanisi.
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments