NGUVU YA AMCOS YAANZA KUONEKANA, KISHAPU NA CHATO WAKO MOTO SANA

 

Muonekano wa mafuta yaliyosindikwa katika Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


 Mhandisi wa Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato, Mashaka Missana akionesha mafuta yalisindikwa katika kiwanda hicho. 
             


Baada ya Vyama Vya Msingi vya Ushirika (AMCO) vilivyokuwa vimesinzia kufufuliwa na kuanzishwa mpya kwenye mikoa kwenye mikoa inayolima zao la pamba, nguvu ya Ushirika imeanza kuonekana.

Wakitembelea Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vinavyolima zao la pamba na alizeti wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na Chato mkoani Geita kwa nyakati tofauti mapema wiki hii, Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo na Waandishi wa habari wameona nguvu ya Ushirika inavyoweza kubadilisha mbinu za uzalishaji na kuchangia maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja na nchi kwa ujumla.

 

Wakiwa katika Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Kishapu mkoani Shinyanga, wamekutana na Trekta ambayo imenunuliwa na AMCOS hiyo kwa fedha taslimu Milioni 35 ambazo zimetokana na kiasi cha shilingi milioni 15 walizopewa mkopo na Benki ya NMB kwa riba ya asilimia 9% mkopo ambao watarejesha ndani ya miaka mitatu, jambo ambalo wamesema liko ndani ya uwezo wao.


“Trekta hili litasaidia kuongeza uzalishaji kwa wanachama wetu, pia tutawalimia wakulima wengine hivyo tutaongeza uzalishaji wa zao la pamba na mazao mengine”,alisema Mwenyekiti wa Kishapu AMCOS, Emmanuel Sona.


“Tumefanikiwa pia kudhibiti ubora wa pamba ambapo sasa wakulima wameachana na tabia ya kuchafua pamba kwa kuongeza mawe, maji na mchanga na vitu vingine. Tunashukuru bei ya pamba iko vizuri na haijashuka kwenye bei elekezi ya serikali shilingi 1560 kwa kilo moja ya pamba lakini tunaomba wanunuzi waje kununua pamba kwa bei ya ushindani”,amesema Sona.

 

Na huko mkoani Geita ,Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) kimeanzisha Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory), wamenunua lori la mizigo, trekta na kujenga ghala la kuhifadhia nafaka kutokana na ushuru walizokusanya na mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).


“Ununuzi wa zana hizi za kilimo umeongeza uzalishaji na kuwapa wananchi unafuu wa upatikanaji wa mafuta,kulimiwa mashamba na kusomba mizigo pamoja ajira”, alisema Katibu wa Chato AMCOS Daudi Mahelule.

Mhandisi wa  Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato, Mashaka Missana akionesha mitambo ya kusindika mafuta katika kiwanda hicho. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mhandisi wa  Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato, Mashaka Missana akionesha mitambo ya kusindika mafuta katika kiwanda hicho
Muonekano wa sehemu ya mitambo katika Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato.
Muonekano wa sehemu ya mitambo katika Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato.
Muonekano wa sehemu ya mitambo katika Kiwanda cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato cha kusindika mafuta ya alizeti (Chato AMCOS Sunflower Oil double refining factory) cha chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Chato.
Na Kadama Malunde 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments