RAIS SAMIA ASHUHUDIA TUKIO LA UWEKAJI SAINI MKATABA UJENZI WA RELI YA KISASA KIPANDE CHA NNE KUTOKA TABORA -ISAKA KM 165

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha nne kutoka Tabora- Isaka km 165 katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Julai, 2022. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa akisaini Mkataba pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Yapi Merkez Bw. Aslan Uzun



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini Mkataba wa Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uendeshaji wa Reli ya Kisasa (SGR). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa akiweka saini pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa KORAIL Bw. Park Tae-hun kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam




    

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha nne kutoka Tabora- Isaka km 165 katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Julai, 2022.

  

Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya utiaji Saini Mkataba wa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka na Mkataba wa Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uendeshaji wa Reli ya Kisasa (SGR)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments