RAIS SAMIA ATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZOTE ZA KOMBE LA YAMLEYAMLE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ametoa vifaa vya michezo kwa timu zote 45 zinazoshiriki mashindano ya kombe la Yamleyamle Zanzibar ili timu ziweze kufanya vizuri hatimaye kuwapata wachezaji bora na wenye vipaji ambao wataunganishwa kwenye timu ya Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa, Julai 3, 2022 wakati akizindua mashindano hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Amani Zanzibar ambapo amesema Mhe. Rais ametoa mipira 45 kwa ajili ya timu hizo na jezi.

“Niwaombe tunapojipanga kwenda kuandaa mashindano ya AFCON, tuleteeni orodha ya vijana wanaofanya vizuri tutahakikisha tunawaingiza kwenye time zetu za taifa, tutawaendeleza, tutakuza vipaji vyao kwa maslahi ya Serikali zote mbili SMT na SMZ”. Amesisitiza Mhe, Mchengerwa.

Amewapongeza kwa kuandaa mashindano hayo ambapo amefafanua kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaandaa mashindano ya AFCON 2027 na kusisitiza kuwa inawezekana iwapo kila mdau atachukua wajibu wake.

Aidha, amefafanua kuwa eneo la soka ndilo eneo pekee ambalo linaweza kuwaunganisha watanzania wote bila kujali itikadi ya dini zao, rangi wala makabila yao.
Na John Mapepele.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments