Serikali Kutoa Ufafanuzi Nyongeza Mishahara, Gumzo Mitandaoni

Serikali ya Tanzania imewataka wafanyakazi kuwa watulivu huku ikahidi kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara ya mwezi Julai, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa kupitia ukurasa wa Twitter usiku wa jana Ijumaa Julai 22, 2022 imeahidi kutolea ufafanuzi suala hilo.

"Ndugu wafanyakazi naomba tutulie, Serikali itatoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara iliyotokea katika mishahara ya mwezi Julai, 2022. Gerson Msigwa. Msemaji Mkuu wa Serikali” imesema taarifa hiyo ya Msigwa bila kueleza lini ufafanuzi huo utatolewa.

msigwa pic2

Mei 14, 2022, Rais Samia Suluhu Hassan aliridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3 ambayo yangeaza katika mshahara wa mwezi Julai.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ilisema mapendekezo hayo ni mwendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichokifanya mkoani Dodoma na kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu kuhusu ongezeko la mishahara.

Taarifa hiyo ilisema Serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh9.7 trilioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.

Nyongeza hiyo ilikuja siku chache baada ya Rais Samia kuwahakikishia wafanyakazi nchini kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 itaongeza mishahara kwa watumishi wake.

 Rais Samia alitoa ahadi hiyo Jumapili Mei Mosi 2022 wakati wa sherehe za wafanyakazi duniani zinazofanyika katika uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma.

Jana, katika ukurasa wa Msemaji Mkuu wa Serikali aliandika kuwa Serikali itatolea ufafanuzi kuhusu nyoingeza ya mishahara ya mwezi Julai.

Hata hivyo, baada ya taarifa hiyo ya Msemaji Mkuu wa Serikali, imeibua mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii ikiwamo baadhi kutoa maoni ‘comments’ kwenye taarifa hiyo.

Baadhi ya mijadala imesema nyongeza ya mishahara ni asilimia 2.33 na sio asilimia 23.3

Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa Twitter anayetambulika kwa ajina la adamlutta @adamlutta alihoji taarifa hiyo ya @TZMsemajiMkuu “Mje na majibu mazuri pia muoneshe na njia kabisa mlivyokokotoa 23% nyongeza ikawa 20k” amehoji

msigwaa pic3

WHYMYCATISSAD @INFLUENCERjr aliandika @TZMsemajiMkuu “Elfu 20 ni nyingi mno yani Njombe unalipa kodi miezi 2”

Pia, NOBODY @excelsior0007 @TZMsemajiMkuu “Oouuh @MabalaMakengeza mimi nilidhani tumeelewana kwenye asilimia.! Kuwa ilikua ni wa kima cha chini..au watu walihisi zile asilimia zinapanda hadi kwa watu wa mamilioni?” alihoji

Abuu @Abuu9777 ambaye aliandika kwa @MsigwaGerson amesema “hamna haja za kufafanua chochote nyie jilipeni mamilioni na wenye mishahara ya digit 6 waacheni wapambane na hali zao , mmejigamba mnaongeza mishahara mnatangaza kila mahali Kisha mtu anakutana na 26000,20000 ,30000 atawaelewa????”

Naye Godlove Emmanuel Ngonde @godlove_ngonde alisema “@MsigwaGerson Kwakweli mama binafsi namkubali Sana. Ila wasaidizi wake sidhani Kama wapo na mama. Na hasa Ile wizara yetu nyeti. Na kwakweli watumishi tumeumizwa pakubwa. Tulijuwa mama anakuja kuyaponya makovu, kilichotokea! Mungu anajua!.”

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments