SHAKA : AWAMU YA SITA IMEIMARISHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

 Wakati akitembelea maonesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam Maarufu kama Saba Saba Leo Alhamisi 6 Julai, 2022.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka amesema CCM inampongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa serikali anayoiongoza kuimarisha na kuboresha mazigara ya biashara na uwekezaji nchini.

Ushahidi umeonekana katika Mwaka wa fedha 2021/22 ambapo makusanyo ya mapato yalikuwa shilingi trilioni 22.28 ikiwa ni ongezeko la sawa na asilimia 113 ya lengo ukilinganisha na makusanyo ya shilingi trilioni 18.15 mwaka wa fedha 2020/2021.

“Chama kimeelekeza katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ibara 49 kwamba serikali itakazounda zitaboresha mazingira na mifumo ya biashara nchini ili kuzalisha fursa za ajira na kuongeza mapato ya serikali. Sote ni mashuhuda wa hatua ambazo serikali inachukua chini ya Rais Samia Suluhu Hassan zinavyozaa matunda ikiwemo biashara kufufuliwa, biashara mpya kufunguliwa na biashara kurejeshwa nchini. Hivyo Chama tunampongeza kwa dhati Mheshimiwa Rais Samia kwa kazi nzuri." Amesema Shaka

Mafanikio hayo yako kwenye uwekezaji pia kwani wawekezaji wameongezeka sana hapa nchini na kwa taarifa za mpaka mwezi Mei, 2022 uwekezaji ulifikia dola za kimarekani dola bilioni 3 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa tangu tupate uhuru.

Shaka amepongeza maandalizi ya maonesho ya mwaka huu ambayo ushiriki umekuwa mkubwa kutoka ndani na nje ya Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa Tantrade Bi. Latifa Khamis alieleza katika maonesho ya mwaka huu makampuni ya kibiashara toka hapa nchini ni takribani 3,000 yameshiriki na kampuni za kibiashara kutoka Nchi 22 duniani yameshiriki ikiwa ni ongezeko kubwa ukilinganisha na maonesho yaliyopita.

Chama Cha Mapinduzi kimewataka watanzania kuendelea kuiamini na kuiunga mkono serikali ili iendelee kufanya mambo mazuri kwa maslahi ya Taifa na wananchi wote ikiwemo kujitokeza kuhesabiwa Agosti 23, 2022.





TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments